Wanafunzi 50 Chuo Kikuu cha Iringa Watimuliwa Baada ya Kudukua Mfumo wa Kulipa Ada

Wanafunzi 50 Chuo Kikuu cha Iringa Watimuliwa Baada ya Kudukua Mfumo wa Kulipa Ada


Jumla ya wanafunzi 50 wanaosoma kozi mbalimbali katika Chuo Kikuu cha Iringa wamelazimika kufukuzwa chuo baada ya kudukua mfumo wa ada na kukisababishia chuo hicho hasara ya zaidi ya milioni 30.

Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Ndelilio Urio amesema kubainika kwa udanganyifu wa wanafunz hao ni mra baada ya kubadilisha mfumo wa malipo kupitia control namba  nakubaini udanganyifu uliojitokeza kwa baadhi ya wanafunzi kughusi malipo na kukiibia chuo ambapo wanafunzi zaidi ya mia mbili walibainika huku baadhi yao wakifutiwa matokeo yao.

Katika hatua nyingine uongozi wa chuo hicho umekanusha tuhuma zilizotolewa na mbunge wa viti maalumu mkoa wa lindi Maimuna Ahmad Pathan, wakati akichangia hoja ya Wizara ya Elimu kwa madai kuwa chuo hicho kina uongozi dhaifu ,mfumo dhaifu wa ulipaji malipo na kuwatoza ada wanafunzi mara mbili.

Akitoa ufafanuzi juu ya tuhumu hizo Makamu Mkuu wa Chuo Profesa Urio amesema chuo hicho kina mfumo wa fedha ambao namba za kufanyia malipo hutengenezwa na kutumwa moja kwa moja kwa mwanafunzi husika kupitia barua pepe yake au namba ya simu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad