Watakaopata Tiketi za bure Mechi ya Yanga USM Alger ni Hawa

 

Watakaopata Tiketi za bure Mechi ya Yanga USM Alger ni Hawa



Mzuka wa pambano la kwanza la fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga na USM Alger unazidi kupanda na mabosi wa klabu hiyo wametoa ufafanuzi wa mgao wa tiketi za bure zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan na makampuni mbalimbali kwa ajili ya mechi hiyo.


Rais Samia amenunua tiketi 5,000, huku Benki ya CRDB nayo ikiunga mkono hamasa hizo kwa kununua tiketi 5,000 pia wakati Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila akinunua 1,000 na tayari baadhi ya walengwa wa tiketi hizo umeanza kugaiwa kupitia matawi ya klabu ya Yanga.


Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe, alizungumza na Mwanaspoti na kusema baadhi ya viongozi walionunua tiketi wameamua kuzigawa katika ofisi zao kama njia ya kutoa furaha kwa watu wanaowaongoza, lakini kwa zile ambazo zipo mikononi mwao watazigawa kuanzia kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu kwani walisahaulika na ni kundi la vijana lenye mashabiki wengi zaidi na wameanza nao .


Kamwe alisema tiketi nyingi zaidi zitakwenda kwenye matawi yote ya Yanga yaliyoko hapa Dar es Salaam na viongozi wa sehemu hizo ndio watakuwa na dhamana ya kuwagawia mashabiki.


"Mashabiki wa timu yetu pekee ndio watakaopata tiketi kwenye matawi na tulichagua zitolewe huko kwa sababu viongozi wanawajua vyema kwani wako nao muda mwingi," alisema Kamwe.


Yanga imetinga fainali ya Shirikisho la Afrika kwa kuitoa Marumo Gallants ya Afrika Kusini kwa jumla ya mbao 4-1 na itashuka Uwanja wa Benjamin Mkapa, Jumapili kwenye mechi ya kwanza kabla ya krudiana nao Juni 3 ili kupata bingwa wa taji hilo lililotemwa na RS Berkane ya Morocco.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad