Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Asimama Masaa 6 Bila Kukaa Akiwasikiliza Wafanya Biashara


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo amesimama kwa saa sita kuanzia saa 5 asubuhi hadi saa 11 jioni bila kukaa akiwasikiliza Wafanyabiashara Kariakoo, yapo mengi ambayo Waziri Mkuu ameyaongea baada ya kuwasikiliza Wafanyabiashara hao, hapa chini nimekuwekea mambo makubwa sita.

1. Waziri Mkuu ameridhia kuunda Tume ya Watu 14 kutoka Serikalini na kwa Wafanyabishara ambao kwa pamoja watashughulikia kero za Wafanyabiashara hao kwa wiki mbili na kupeleka mapendekezo Serikalini.

2. PM Majaliwa amesisitiza kuondolewa kwa task force ambazo amesema zinanyanyasa Wafanyabiashara na Vijana wa task force kuchukua rushwa.

3. PM Majaliwa amekemea tabia ya Viongozi kudharau maagizo ya Rais na amesema atakayesema maagizo ya Rais ni ya kisiasa jina lake litajwe ili achukuliwe hatua.

4. PM Majaliwa amewataka Polisi wasikusanye kodi kwakuwa sio jukumu lao.

5. Kuhusu tozo za stoo, PM Majaliwa amekiri kuna dosari kwakuwa sheria inayosimamiwa na TRA sio mbaya lakini kuna kanuni hapa amezisitisha na kusema Kamati iliyoundwa itapitia kwa kina kujua tatizo lipo wapi.

6. PM Majaliwa mara nyingine tena amewaomba Wafanyabiashara wa Kariakoo wakubali kufungua maduka yao ili biashara iendelee kama kawaida ambapo amesema Kamati iliyoundwa leo yenye uwakilishi wa Wafanyabiashara pia itahakikisha malalamiko yote yanafanyiwa kazi.

Baada ya ombi hilo la Waziri Mkuu Wafanyabiashara wameonekana kukubali kwa kupiga makofi huku wakiahidi kufungua maduka.
#MillardAyoUPDATES
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad