Waziri Mkuu Majaliwa aunda Kamati, ‘Mgomo Kariakoo’




Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametangaza kuunda Kamati maalum inayoundwa na Viongozi wa Serikali, Wafanyabiashara na Viongozi wa TRA ili wapite kwenye masoko ya Dar es salaam na Mikoani na kukutana na Wafanyabiashara ili kukusanya maoni yao na kuyawasilisha Serikali yapatiwe ufumbuzi.

Upande wa Wafanyabiashara umewakilishwa na Wajumbe ambao majina yao yamependekezwa na Wafanyabiashara wenyewe kwa uwazi kabisa akiwemo Vunja Bei, Mama Bonge, Kiongozi wa Wafanyabiashara Tanga, Mwenyekiti wa Wafanyabishara Kariakoo na Mwakilishi wa Wafanyabishara Zanzibar.

Waziri Mkuu amesema “Hawa Wajumbe wa Kamati watakwenda kwenye Masoko yote ya Dar es salaam na Mikoa mingine yote ili wakutane na Wafanyabiashara na Taasisi za Serikali na wana uwezo wa kumuhoji yoyote ili wapate maoni ambayo yatawasilishwa kwa Serikali na kwa Rais Samia”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad