Wema Sepetu Afunguka "Nilimwacha Diamond Platnumz 'alinichiti"

 

wema na diamond

Muigizaji na mwanamitindo kutoka Tanzania Wema Sepetu amefunguka kuhusu kuachana na staa wa Bongo Diamond Platnumz.


Akihojiwa na kituo cha runinga cha Manara, dada huyo ambaye aliwahi kushinda taji la Miss Tanzania alisema alimtoka mwanamuziki huyo kwa sababu ya tabia za kuchiti.


Wema alidai kuwa hakun siku alimchezea nyota huyo wa kibao cha Mawazo, kwani alikuwa mwaminifu siku zote. Alisema alikuwa amechoka kukabiliana na tabia yake ya kuchepuka na ndiposa akaamua kumtema.


“Nilikuwa nimechoka, nilikabiliana na masuala ana kwa ana, nikishughulikia yale ambayo yalihitaji kushughulikiwa, lakini mwishowe niliamua kuachana na Diamond. Nilikataa hata zawadi yake ya gari mbele ya wengine kwa sababu singeweza kuvumilia tena vitendo vyake vya usaliti,” Wema alisema.


Ufichuzi huu wa hivi punde unazima uvumi kuwa mastaa hao wawili walitengana kwa sababu Wema hakuweza kushika mimba.


Hapo awali, mwigizaji huyo nyota alifichua kwamba alifanya mapatano ya damu na Diamond Platnumz walipokuwa bado pamoja.


Katika mahojiano ya hivi karibuni na kipindi cha udaku nchini Tanzania, Chumba Cha Umbea, Wema alimzungumzia Diamond kwa kusema kuwa mwimbaji huyo anathamini mapenzi na alikuwa kila kitu kwake.


“Diamond ni mwanaume anayeabudu mapenzi, alikuwa kama mtoto wangu, namaanisha kama wa kwangu kabisa,” Wema alisema kwa sauti iliyoonyesha ni kiasi gani alimaanisha maneno yake.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad