Wema: Sijakata Tamaa Kupata Mtoto, Natumia Mitishamba

 

Wema: Sijakata Tamaa Kupata Mtoto, Natumia Mitishamba

Wema Sepetu "Nilinenepa kwa sababu nilikuwa natumia vidonge ili nipate mimba, lakini matokeo yake nilijikuta nanenepa kama puto na mimba sipati, iliniumiza sana nilinenepa kiasi kwamba hata kutembea kutoka sebureni kwenda chumbani ilikuwa shida, nilivyoona hakuna matokeo ndipo nilipoanza kufanya jitihada za kujikondesha ili nibaki na mwili wa kazi yangu ya uigizaji.


"Pamoja na kwamba nimekonda lakini bado sijakata tamaa, bado natumia dawa za miti shamba, nimekuwa kama mtumwa wa hizi dawa naamini ipo siku Mungu atanibariki mtoto maana mimi kama mtoto wa Kiislamu pia nakesha kuomba Dua ipo siku Inshaallah, matumaini yangu ni kwamba ipo siku nitapata mtoto lakini ikitokea Mungu akininyima kabisa nitaumia sana, nitaathirika sana kisaikolojia.


"Kuhusu kupata pesa nyingi kipindi cha nyuma kisha kuzitumia vibaya kwa anasa na kuwatunza marafiki ambapo baadae pesa ziliisha bila kujenga hata nyuma moja, Wema amejitetea kwa kusema.


"Ni kweli mimi nimeshika pesa nyingi sana kipindi cha nyuma, lakini hazikupotea kwa anasa kama watu wanavyodhani, nilipoteza Milioni 320 kwenye kampeni mwaka 2015 nilipogombea Ubunge, nilitumia pesa nyingi kwasababu mategemeo yangu nilijua nitashinda lakini nilijikuta nimeteketeza pesa nyingi na Ubunge nikakosa, iliniaumiza sana.


"Mimi nina kawaida moja, sina presha na maisha, nikipata natumia na nikikosa naridhika maana najua kwenye maisha kuna kupanda na kushuka, kupata na kukosa na ninaamini kila kitu kinatokea kwasababu kwahiyo hilo suala la mimi kupungua kifedha halinipi shida hata kidogo maana najua kuridhika na halinipunguzii mimi kuwa Wema Sepetu.


"Kama ulikuwa unajua Wema ndiyo chanzo cha Penzi lake na Diamond Platnumz kuvunjika basi kwa mara ya kwanza leo Wema ameweka ukweli mezani.


"Mimi na Naseeb (Diamond Platnumz) tuliachana kwa sababu alinichiti, na hakunichiti mara moja au mara mbili, alinichiti mara nyingi sana kiasi kwamba kama binadamu kuna muda unashindwa kuhimili mikiki-mikiki unachoka unaondoka.


"Tulishakaa vikao vingi vya familia kuisaka suluhu lakini baadae ilifika mwisho, na mimi sikuwahi kumchiti hata siku moja ila yeye ndiye alikuwa kinara wa kuchepuka," amesema Wema Sepetu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad