Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema klabu imeanza mchakato wa ujenzi wa uwanja eneo la Jangwani yalipo Makao Makuu ya klabu ya Yanga
Akizungumza katika kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM, Injinia Hersi alisema taratibu za awali zimeshaanza kufanyika hapo Jangwani
"Kuhusu ujenzi wa Uwanja tuna kiwanja Kigamboni lakini pia tuna eneo ambalo lina jengo la Klabu pale Jangwani, sisi binafsi tumependelea kujenga uwanja wetu pale Jangwani na tayari taratibu zimeshaanza katika kulitekeleza hilo," alisema Hersi
Ujenzi wa uwanja ilikuwa moja ya ajenda za Injinia Hersi wakati akigombea Urais wa klabu ya Yanga
Moja ya sababu ambayo Hersi aliitaja kujenga uwanja pale Jangwani badala ya Kigamboni ambako Yanga ina eneo kubwa zaidi, ni urahisi wa kufikika kwa mashabiki
Hersi alisema wataalam waliwathibitishia kuwa katika eneo lao la uwanja wa zamani wa Kaunda, wanaweza kujenga uwanja wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 20,000