Young Africans yamshitaki Fei Toto kamati ya nidhamu




Kamati ya Nidhamu ya Klabu ya Young Africans imethibitisha kupokea malalamiko ya Uongozi wa Klabu hiyo dhidi ya Kiungo kutoka Zanzibar Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’.

Kwa miezi sita sasa Fei Toto amekuwa katika mgogoro na Uongozi wa Klabu ya Young Africans, baada ya kushinikiza kuvunjwa kwa mkataba wake mwishoni mwa mwaka 2022.

Kamati ya Nidhamu ya Young Africans imethibitisha kupokea malalamiko ya Uongozi, kupitia barua rasmi aliyoandikiwa Fei Toto, akitakiwa kufika mbele ya Kamati hiyo ili kujitetea kwa makosa ya kinidhamu.

Barua aliyoandikiwa Fei Toto imeeleza: Kamati ya Sheria na Nidhamu ya Young Africans Sports Club imepokea malalamiko kutoka kwa uongozi wa Klabu inayo kutuhumu kwa makosa mbali mbali ya kinidhamu kama yalivyoainishwa kwenye Hati ya Mashtaka ambayo imeambatanishwa kwenye barua hii.


Unaelekezwa kuwasilisha utetezi wako juu ya tuhuma zinazokukabili kama zilivyoainishwa kwenye Hati ya Mashtaka ndani ya siku saba (7) tangu tarehe ya barua hii na kutuma utetezi wako katika anuani ifuatayo:

Kamati pia inakuelekeza kuhudhuria kikao cha Kamati ya Sheria na Nidhamu kitakacho sikiliza mashtaka dhidi yako mnano tarehe 24 Mei 2023 saa 4:00 Asubuhi katika Ofisi za Klabu zilizopo Jangwani ukumbi wa mikutano ukiwa pamoja na mwakilishi wako (iwapo utapenda kuwa na mwakilishi) ili kukusikiliza wewe pamoja na Mlalamikaji na kufanya maamuzi juu ya tuhuma zinazokukabili.

Fahamu kwamba kushindwa kwako kuwasilisha utetezi wa maandishi dhidi ya tuhuma zinazokukabili ndani ya muda uliotajwa au kutofika kwenye kikao kutafanya kamati iendelee na Kikao bila uwepo wako.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad