Zari Amchana Diamond Vibaya Sana 'Sikuhitaji Tena, Mimi Ndio Nilikutambulisha East Afrika Yote Ikakujua'


Mrembo kutoka Nchini Uganda na Mzazi Mwenzake na Staa wa Muziki @diamondplatnumz , #ZARITHEBOSSLADY Ameamua kumvulia Uvivu staa huyo baada ya kutokupendezwa na alichokifanya #Diamond kwenye Show ya Young, Famous & African.
.
Kupitia ukurasa wa #Zari ameandika mengi akionesha kutokupendezwa na aliyoyafanya Staa huyo huku akimwambia kuwa kwa sasa ana mahusiano yake na asitegemee kama atarudiana nae.

"Mpendwa Ex
Ninakuheshimu sana kama baba wa watoto wangu na hakuna kinachoweza kuingilia kati kwenye hilo. Ikiwa kungekuwa na nafasi ya sisi kurudi pamoja ungerudi mbio. Jinsi umekaa na madada Poa (watu wa muda katika maisha yako) wakijadiliana kuhusu mimi hainishangazi,Unaweza kumchumbia mtu yeyote unayemtaka bila kunitumia kama njia Sikuhitaji Nina busara tu kwa sababu ya watoto, Watoto wanagoggle vitu vingine naweza kuvielezea vingine nashindwa,Umefanya ingizo ambalo halikuwepo kwenye Mpangilio na umesema uongo kunihusu jinsi ninahitaji kukaa na wewe na watoto,Ninavyovutiwa na wewe ,Wewe ni nani kwa Zari the Boss lady utakuwa karibu na mimi kwa sababu ya watoto na kama hupendi acha mahakama iamue,Afrika Mashariki nzima haikukujua mpaka nilivyokutambulisha Wewe ni DIAMOND, unaweza kupata mtu yeyote unayemtaka bila kunishirikisha.
Mimi ni mwanamke niliyeolewa kwa sasa na uchafu wako haujakaa vizuri kwenye ndoa yangu. "





Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad