Zitto, Nondo watoa ya moyoni kifo cha Membe





Dar es Salaam. Mwanasiasa Zitto Kabwe ametuma salam za rambirambi kwa familia ya Benard Membe aliyefariki asubuhi ya leo  akieleza jinsi alivyomfahamu na kufanya kazi na mwanasiasa huyo.

Zitto ambaye ni kiongozi Chama cha ACT Wazalendo ametaja Membe ambaye aliwahi kuwa mwananchama wa chama hicho kama mwanasiasa mahiri.

Membe ambaye alikuwa mwanachama wa CCM alijiunga ACT Wazalendo Julai 15 mwaka 2020 kisha kurejea CCM Mei 29 mwaka 2022.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Zitto ameandika, “Hakuna maneno yanayoweza kueleza mshtuko mkubwa nilioupata kufuatia taarifa ya msiba huu, zaidi ya kumshukuru Mungu muumba kwa maisha ya mzee wetu Bernard Membe ambaye amefariki dunia leo asubuhi. Mwanasiasa mahiri, mwanadiplomasia maarufu na mwakilishi wa wananchi.


“ Kwa niaba yangu Binafsi na kwa niaba ya Wanachama wa Chama cha ACT Wazalendo ambaye BM aliwahi kuwa mwanachama wake natoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wananchi wote wa Jimbo la Mtama @Nnauye_Nape na Mkoa wa Lindi @Isihakamchinji1 kufuatia msiba huu mkubwa. Tupo pamoja katika kipindi hiki cha majonzi,”ameandika Zitto.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Ngome wa Vijana wa chama hicho, Abdul Nondo ameeleza namna Membe alivyokuwa mlezi kwake kwenye siasa.

“Innaillah Wainalailah Rajeun, nimepoteza mtu muhimu sana.Mungu akulaze mahali pema Mzee wangu, Bernard Membe. Kwangu wewe ulikuwa ni mzazi, mlezi na mshauri wangu katika siasa ukiwa ndani ya chama chetu hata nje ya chama chetu uliendelea kunielea, siamini leo umetuacha,” ameandika Nondo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad