Abdul Misambano 'Nilibadili rangi ya ngozi yangu sababu nilichoka kuwa mweusi'

 

Abdul Misambano 'Nilibadili rangi ya ngozi yangu sababu nilichoka kuwa mweusi'

Msanii maarufu wa muziki wa taarabu anayehudumu kwenye kikundi cha T.O.T chini ya Malkia Khadija Omar Kopa, Abdul Misambano amewatolea uvivu walimwengu wanaomsakama baada ya ngozi yake kuonekana imeharibika kutokana na kujichubua.


Misambano ambaye mpaka sasa yupo singo baada ya mke wake kumkimbia na kwenda kuolewa sehemu nyingine amesema aliamua kubadilisha rangi yake baada ya kuuchoka weusi, anasema watu waelewe kitu kimoja kwamba yeye hapaki mkorogo bali kuna mafuta maalumu ambayo anayapaka ambayo ndiyo yamemfanya atoke kwenye weusi na kuwa mzungu.


Ameongeza kuwa hajaanza kujichubua leo wala jana, alianza kujichubua tangu enzi za Mwinyi akiwa madarakani.


Kuhusu uso wake kubabuka, Misambano amesema ilitokea bahati mbaya aliuziwa kipodozi kilichoisha muda wake ambapo baada ya kujipaka ndiyo kikamletea madhara ya kubabuka ngozi na kuwa na weusi wa mkaa kwenye engo za mashavu, ingawa kwa sasa anaendelea vizuri na amesema haachi kujikoroga leo wala kesho.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad