Ahmed Ally: Kiatu Cha Mfungaji Bora ni cha Saido, Sababu ni Hizi Hapa

 

Ahmed Ally: Kiatu Cha Mfungaji Bora ni cha Saido, Sababu ni Hizi Hapa

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Club ya Simba Ahmed Ally amesema Mchezaji wa Simba Saido ndio anastahili kuwa Mshindi wa Tuzo ya Mfungaji bora msimu huu kwakuwa amecheza mechi chache (23) kuliko Mayele aliyecheza mechi 26.


Ahmed ameandika; “Mwaka 2012 kwenye mashindano ya UEFA EURO CHAMPIONS LEAGUE Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Hispania Fernando Torres alitwaa tuzo ya Mchezaji bora licha ya kuwa na idadi sawa ya magoli na Mshambuliaji Mario Gomez wa Ujerumani”


“Kigezo kilichotumika kumpa Torres kiatu cha dhahabu ni kuwa alicheza dakika chache kulinganisha na Gomes na pia Torres alikua na assist moja wakati Gomes hakua nayo, Mayele amecheza mechi nyingi 26 amefunga magoli 17, Saidoo amecheza mechi chache 23 amefunga 17 na asisst kama zote 12.


“Kwa mantiki hiyo Saido ndo mfungaji bora msimu huu kwani kama angecheza mechi sawa na Mayele angekua na magoli mengi,” amemalizia Ahmed.


Mtazamo wako ni upi ? nani apewe Tuzo ya Mchezaji bora kati ya Mayele na Saidoo?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad