Aliyekuwa Mchezaji Chelsea Afilisika Vibaya Hana hata pa Kulala wala Kula


Katika ubora wake akiwa kijana mwenye umri wa miaka 20 Jacob Alexander Mellis aliitumikia Chelsea kwenye michuano ya Klabu Bingwa Ulaya na kulipwa takribani Pauni 8000 kwa wiki, lakini hivi leo hana mahala pa kuishi.

Kwenye mahojiano na Gazeti la Daily Mail, Mellis mwenye umri wa miaka 32 ameweka wazi hali ngumu ya kimaisha anayopitia baada ya miaka mingi hapo nyuma kutabiriwa makubwa wakati akiitumikia academy ya Chelsea.

Hivi sasa Mellis hana mahala pa kuishi, hana gari na hana kipato. Kwa muda wa miezi 18 iliyopita, amekuwa akitegemea huruma ya familia na marafiki ambao wamekuwa wakimpatia sehemu ya kulala na mara nyingine pesa ya chumba cha hoteli.

Kustaafu mapema kumemfanya Mellis kujikuta kwenye matatizo mengi sana. Jeraha la goti alililopata akiitumikia klabu ya Southend, lilikatisha kipindi cha miaka 13 iliyoanzia Stamford Bridge, ambapo mechi yake ya kwanza ilifanyika kwenye Ligi ya Mabingwa dhidi ya timu ya Slovakia, MSK Zilina.

Mellis alikiri kwamba hakutumia vyema uwezo wake, tabia ya kutanguliza unywaji pombe na kuparty usiku kucha ilififsha ndoto zake.

Mellis alisema “Nakumbuka kipindi nikiwa Chelsea wakati mmoja nilifika kwenye mazoezi nikiwa nimelewa. David Luiz ambae hakuzungumza sana Kiingereza alinionya kuhusu tabia hiyo ya ulevi”.

“Nilikuwa mjivuni wakati huo, mwenye kiburi. Nilihisi kama napaswa kucheza. Kama sikupangwa nilihisi kuchanganyikiwa, hivyo nilitoka kwenda kunywa. Ukweli ni kwamba sikuikomoa Chelsea, nilijiharibia mwenyewe.”

“Wakati nacheza sikuona tatizo lolote, lakini baada ya kustaafu nimeanza kujuta sana, watu wanashangaa na kuuliza nini kimenikuta”.

Chama cha wachezaji wa kulipwa “PFA” kimeonyesha nia ya kumsaidia kupambana na tatizo lake la ulevi, lakini pia klabu ya Chelsea imemsaidia Mellis kupata kozi zake mbili za kwanza za utambuzi wa vipaji huku akilenga kurejea kwenye soka.

Mellis alimalizia kwa kusema kuwa “Natazama soka siku nzima, kila siku. Ninapenda kuona
vipaji vya vijana wanao chipukia. Nahisi kama ninaweza kuwasaidia nje ya uwanja kwa kuwaelekeza njia za kupita ili wasirudie makosa yangu”.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad