Amina Mke wa Mwanamuziki Ali Kiba Aomba Talaka Yake

 

Amina Mke wa Mwanamuziki Ali Kiba Aomba Talaka Yake
Ali Kiba na Mkewe

Amina Khalef kutoka Kenya, mke wa Alikiba, adai kuchoshwa na tabia za kuvunjiwa heshima hadharani ambazo anatendewa na mumewe huyo.


Amina ameweka wazi hisia zake kupitia insta story ambapo amesema;


"Nimeona kuna haja ya kulizungumza, nafikiri hii imezidi. Nimechoshwa kuvunjiwa heshima hadharani huku watu wakiwa hawaelewi hali iliyopo katika kivuli cha mke wa mtu".


"Nimeondoka kwenye maisha yako kuepuka maumivu, unyanyasaji na mengine mengi lakini mpaka leo hutaki kunipatia Talaka huku wewe [Alikiba] ukiwa huru kufanya mambo yako na mimi ukinifunga katika kivuli cha mke wa mtu".


"Kimsingi naomba usaini karatasi ili nipate Talaka kila mmoja aendelee kuwa huru".


Ndoa ya King Kiba na Bi. Amina ilifungwa mwezi Aprili, 2018 na kubahatika kupata watoto wawili, Keyaan Kiba na Kamran Kiba.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad