Anayedai Mtoto wa Mzee Yusuf ajitokeza, Mwenyewe Amkana

Anayedai Mtoto wa Mzee Yusuf ajitokeza, Mwenyewe Amkana




Kijana mmoja aliyejitambulisha kwa majina ya Ahmad Yusuph Mzee, amejitokeza hadharani katika studio za Wasafi Media akidai kwamba yeye ni mtoto wa mzee Yusuph wa damu kabisa ambapo anasema kwamba mama yake ambaye ni Marehemu kwa sasa alipewa ujauzito na Mzee Yusuph wakati alipokuwa akihudumu kama MC kwenye moja ya kumbi iliyokuwa huko Mbagala miaka ya 2002.


Ahmad anasema awali alikuwa akiishi na mama yake pamoja na mume wa mama yake ambaye awali alikuwa anamtambua kama baba yake mzazi, lakini kabla mama yake hajafariki alimweleza ukweli kwamba hakua baba yake wa kumzaa bali baba yake ni Mzee Yusuph ambaye ndiye huyu muimba taarabu.


Ahmad amesema licha ya kwamba anatambua kama Mzee ana mali za kutosha na ni mtu maarufu, yeye kipaumbele chake anataka wakapime DNA ajiridhishe kama kweli Mzee Yusuph ni baba yake mzazi ili awe na faraja pamoja na amani ya kujihisi yupo salama duniani kwani kwa maisha anayoishi sasa ni kwamba hana baba wala mama, maisha ambayo ni hatari na siyo kwamba anamtafuta ili apate upenyo wa kurithi mali.


Kwa upande wa Mzee Yusuph licha ya kufanana na mtoto huyo kuanzia Mapua, Mdomo, Mashavu, kichwa mpaka rangi ya meno na ngozi.


Bila aibu Mzee amesema hamtambui kijana huyo kama mtoto wake na hana kumbukumbu kama aliwahi kucheza michezo ya hasara huko Mbagala kiasi cha kumpatia mwanamke ujauzito.


Awali Mzee Yusuph alikataa kabisa kupima DNA lakini baadae baada ya kushinikizwa alikubali kwenda kupima DNA lakini kwa masharti mazito, ambapo amesema kijana huyo akitaka wakapime DNA pesa ya vipimo aitafute mwenyewe kijana na andapo atakuta siyo mtoto wake basi hatua kali za kisheria za uzalilishaji zitachukuliwa dhidi yake.


Aidha, Yusuph ameongeza kuwa kama akikuta mtoto huyo ni damu yake atamfikilia kama aendelee kumlea au aachane naye kwani dini yake inasema mtoto wa nje ya ndoa siyo mtoto wake ni wa mwanamke.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad