Azam yafunguka kuhusu kumshawishi Fei Toto



Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC Abdulkarim Nurdin Amin ‘Popat’ ameshauri kumalizwa kwa hali ya usalama na Amani sakata la Kiungo kutoka visiwani Zanzibar Feisal Salum ‘Fei Toto’ ambaye amedhamiria kuvunja mkataba na Klabu ya Young Africans.



Kiungo huyo amekwama katika mpango huo kwa zaidi ya mara moja mbele ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ ambapo mara ya mwisho alitakiwa kukaa chini na Uongozi wa Young Africans ili kumaliza sakata hilo.

Akizungumza na TBC FM Popat amesema sakata la Kiungo huyo limefikia hatua linaonekana kama kuna uadui kati yake na Uongozi wa Young Africans, halia mbayo sio nzuri kwa ustawi wa Soka la Tanzania.

"Azam FC ni miongoni mwa klabu zilizosajili Wachezaji wengi msimu huu, na Wachezaji wengi wameonesha kiwango kizuri hivyo hatutasajili sana msimu ujao"

"Tutasajili Wachezaji watatu tu na tayari tumeshasajili Wachezaji wawili. Tulimruhusu Sure boy aondoke akiwa kabakiza miezi 8, tulimruhusu Gadiel Michael akiwa bado na Mkataba, mpira sio Uadui.

"Inasemekana nyie ndio mliomshawishi Feisal aigomee Yanga" - Steven Mumbi Mtangazaji.

"Sisi hatuwezi kufanya kitu kama hicho," amesema Popat.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad