Baada Ya Kuachwa… Mkude Atoa Tamko Zito Simba, Amtaja MO Dewji



MARA baada ya kutangazwa rasmi kutokuwa sehemu ya Simba kwa msimu ujao, aliyekuwa kiungo wa timu hiyo, Jonas Mkude amefunguka kuwa anawashukuru Simba kwa sapoti waliyompa katika kipindi chote cha maisha yake na kuwatakia kila la kheri.

Mkude alitangazwa rasmi kutokuwa sehemu ya kikosi cha Simba kwa msimu ujao juzi Alhamisi baada ya kumaliza mkataba wake na timu hiyo, huku akiwa na rekodi ya kuitumikia kwa kipindi cha miaka 13 akitokea kwenye kikosi cha vijana U20.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Idara ya Habari ya Simba, Mkude alisema: “Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru sana viongozi, mashabiki na wachezaji wenzangu ambao tumefanikiwa kufanya kazi kwa kipindi kirefu pamoja.


“Kama mchezaji mwandamizi najivunia mafanikio ambayo nimefanikiwa kuyapata nikiwa hapa, licha ya kwamba inawezekana yasiwe makubwa sana lakini kama mchezaji yametengeneza rekodi kubwa katika historia ya maisha yangu na Simba.


“Kwa pekee sana napenda kumshukuru kocha Seleman Matola na meneja Patrick Rweyemamu ambao ndio waligundua kipaji changu na kunileta Simba, lakini pia namshukuru aliyekuwa Mwenyekiti wetu Godfrrey Nyange ‘Kaburu’ pamoja na mwekezaji wetu, Mohammed ‘Mo’ Dewji kwa kunipambania mpaka mwisho. Kwa Wanasimba nawapenda wote na mpaka wakati mwingine.”

Stori na Joel Thomas

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad