Africa music wonder kid, Kelvin Kioko Bahati (@bahatikenya) amemchumbia Diana Marua kwa mara ya pili, atangaza rasmi tarehe ya harusi na mpenzi wake huyo wa muda mrefu.
Mkali huyo kutoka Kenya ametumia ukurasa wake wa instagram kutoa habari hii njema kwa kuandika; "Amesema ndio, rasmi na tangaza kuwa Disemba 12,2023 itakuwa siku yetu ya harusi".
Muda mfupi baadae @diana_marua nae alitoa shukrani zake za dhati kwa Baby Daddy wake huyo kwa upendo na thamani anayo mwonesha.
Mwaka 2017, mwezi Oktoba taarifa zilienea kuwa msanii huyo amefunga ndoa na Diana kimya kimya na baada ya mazungumzo na MondayBlues, Bahati alisema tukio hilo lilikuwa la Kifamilia na linajulikana kama ruracio na sio harusi kamili, kama watu walivyodhani.
Msanii huyo wa zamani wa muziki wa Injili ana watoto watano, ambapo watatu wa kuwazaa Diana na wengine wa wawili aliwa-adopt kutoka kituo cha Watoto cha ABC kama sehemu ya kurudisha kwa jamii.