Baada ya Kupigwa Chini Usambazaji wa JEZI Simba, Vunja Bei Aibuka na Kusema Haya

 

Baada ya Kupigwa Chini Usambazaji wa JEZI Simba, Vunja Bei Aibuka na Kusema Haya

Mkurungezi wa Kampuni ya Vunjabei Fred Ngajilo ametoa Shukrani kwa Klabu ya Simba Sports Club kwa kumuamini na kufanya nae kazi kwa Miaka Miwili huku akisema kuwa wameleta mapinduzi makubwa kwa Tasnia ya Utengenezaji na usambazaji wa Jezi na vifaa vya Michezo, Kupitia ukurasa wake wa Instagram #Fred ameandika….

“Verified Menejimenti ya Vunjabei (T) Group Limited inapenda kutoa shukrani za dhati kwa bodi ya wakurugenzi, menejimenti, benchi la ufundi, wachezaji, wanachama na mashabiki wote wa Simba Sports Club kwa ushirikiano mkubwa ambao wamekuwa wakitupa katika kipindi chote cha miaka miwili ambayo tumefanya kazi ya Mapinduzi makubwa ya tasnia hii ya utengenezaji na usambazaji wa vifaa vya michezo.

Tunatarajia kuendelea kudumisha uhusiano huu tulioujenga, tunachukua fursa hii kumpongeza mzabuni mpya na hatutasita kumpa ushirikiano wa aina yeyote pale tutakapohitajika.

Tunaamini kuwa tutaendelea kufanya kazi kwa pamoja ili kuelekea kwenye mafanikio zaidi na kusababisha maendeleo katika mpira wetu wa miguu Tanzania.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad