Baba wa Mwanamuziki 2 Pac Atoboa SIRI Nzito "Mauaji ya 2 Pac Yalipangwa na Serikali'

Baba wa Mwanamuziki 2 Pac Atoboa SIRI Nzito "Mauaji ya 2 Pac Yalipangwa na Serikali'


Billy Garland, baba mzazi wa the late Tupac Shakur amedai kuwa mauaji ya mwanae yaliyotokea mwaka 1996 yalipangwa na serikali ya Marekani.

Garland aliendelea kusema kuwa alikuwa anafahamu kuwa mjomba wa Anderson, Duane ''Keefe D'' Davis, alikuwa amekiri mbele ya serikali ya Marekani kuwa alifyatua risasi zilizosababisha kifo cha mwanae.

Orlando Tive ''Baby Lane'' Anderson (Mpwa wake Keefe D) kwa muda mrefu amekuwa mtuhumiwa mkuu katika mauaji ya 2Pac.

''Ninadhani swali muhimu hapo ni serikali. Serikali ilimpa makubaliano. [2Pac] alikuwa akiandamwa na serikali usiku wa mauaji yake. Alifuatiliwa na serikali akiwa studio, huo ni ukweli uliojulikana.''

''Kwa hivyo simjui mtu huyu Keefe, simjui. Labda alilazimika kusema hivyo ili kujiondoa kwenye suala fulani, sijui''

''Ninajua tu ilionekana kama mpango kwangu. lakini sidhani kama [Orlando Anderson] alikuwa na uhusiano wowote na kifo cha mwanangu……hata kidogo.''

Tupac Shakur alifariki tarehe 13 Septemba 1996, siku sita baada ya kupigwa risasi karibu na eneo la Barabara ya East Flamingo na Koval Lane huko Las Vegas. Alikuwa na umri wa miaka 25 tu.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad