Bakwata yatangaza sikukuu Eid El- Adha, kufanyika Alhamisi Juni 29 mwananchi.co.tz




Dar es Salaam. Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (Bakwata) limetangaza kuwa Sikuku ya Eid El-Adh'haa itakuwa Juni 29 mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa na baraza hilo na kusainiwa na Katibu Mkuu wa baraza hilo Alhaj Nuhu Mruma imeeleza kuwa sherehe za Eid El-Adh'ha kitaifa kwa mwaka huu zitafanvika Mkoa wa Dares Salaam.

“Swala ya Eid itaswaliwa katika Msikiti wa Mfalme Mohamed VI Bakwata Makao Makuu Kinondoni kuanzia saa 1.30 asubuhi na kufuatiwa na Baraza la Eid mara tu baada ya Swala.

Kwa niaba ya Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Abubakar Zubeir bin Ally Mbwana anawatakia Waislamu na wananchi wote maandalizi mema ya Sikukuu hiyo,” imeeleza taarifa hiyo ya Mruma.


Eid El-Adh'ha ni sikukuu ambayo huadhimishwa baada ya Waislamu kukamilisha ibada ya Hijja ambayo ni nguzo ya tano katika nguzo za Uislamu.

Nguzo ya kwanza ni shahada ambayo Muislamu anapaswa atoe shahada kwa kusema kwamba nakiri kuwa hakuna Mungu isipokuwa Allah na kwamba Muhammad ni mjumbe wa Allah.

Nguzo ya pili ni kuswali swala tano ambazo zimewekewa nyakati maalumu alfajiri, adhuhuri, alasiri, magharibi na ishai (usiku).


Kwa imani ya Uislamu Mtume Muhammad (S.A.W) alipewa amri ya umati wake kuswali wakati alipokwenda Miiraj (safari ya muujiza aliyokwenda Mtume S.A.W kutoka Makka kwenda Baitil Maqdis iliyopo Palestine).

“Ametakasika, aliyemchukua mja wake usiku mmoja kutoka Msikiti Mtukufu mpaka msikiti wa mbali, ambao tumevibariki vilivyouzunguka, ili tumwonyeshe baadhi ya ishara zetu...” (Al-Israa 17: 1).

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad