Akitoa taarifa za awali Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe, Kamanda John Makuri Imori, amesema ajali hiyo imetokea leo Juamtano, Juni 21, 2023 majira ya saa 8:30 mchana wakati basi hilo likitoka jijini Dar es Salaam kwenda Sumbawanga, mkoani Rukwa.
Aidha, Kamanda Imori ambaye bado yupo eneo la tukio amesema chanzo cha ajali hiyo ni basi la New Force baada ya kufika eneo la Igando, sehemu ya daraja, dereva alikawa akitaka kulipita (overtake) ndipo likapoteza muelekeo na kutumbukia mtaloni.
Endelea kufuatilia Tanzaniaweb.com kwa taarifa zaidi.