Mlinda Lango wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Beno Kalolanya, amesema kwenye Ligi Kuu Tanzania anafurahishwa mno na wachezaji wawili, kipa wa Young Africans Djigui Diarra na kiungo mshambuliaji wa Simba SC Clatous Chama, huku akitaka wachezaji wa Kitanzania wajifunze baadhi ya vitu kutoka kwao.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Kakolanya ambaye amemaliza mkataba wake na Simba SC na sasa anatarajia kujiunga na moja kati ya timu kubwa hapa nchini kwa mujibu wake, amesema nchi yetu imebahatika kuwa na aina hiyo ya wachezaji na ni jambo jema kwa wachezaji wa Kitanzania wakaangalia baadhi ya vitu ambavyo vinaweza kuwasaidia na kuwa somo kwao.
“Wachezaji ambao ninawakubali mimi kwenye ligi ya Tanzania ni kipa Diarra, hata mimi kuna vitu najifunza kutoka kwake, anajua kuanzisha mpira, anaweza kuwatoa wachezaji wawili wasiwe kwenye mchezo na kuanza na mabeki, unajua ile inaanzia utotoni, yale ni mafunzo kabisa, wenzetu wamepata bahati hiyo.
Gamondi afunguka atakapoifikisha Young Africans
“Makipa wengi Tanzania tunajua kudaka tu, lakini tunakosa baadhi ya vitu kama vile kwa sababu hatukupata mafunzo sahihi ya ukipa tangu tukiwa wadogo, tukiona vitu kama vile inatakiwa tuvichukue, mimi kuna vitu nimechukua kutoka kwake,” alisema kipa huyo wa zamani wa Prisons na Yanga.
Amesema mchezaji mwingine ni Chama, aliyemtaja ni mmoja ya wachezaji wa kiwango cha hali ya juu Afrika anayecheza Ligi ya Tanzania.
Achraf Hakimi kurudi Real Madrid
“Nchi imebahatika kuwa na wachezaji kama Chama na ligi yetu pia imepata bahati hiyo, kwa wachezaji vijana wasiache fursa ya kujifunza kutoka kwake, ni wa aina yake, namkubali sana,” amesema