BUNGENI: Waziri Mbalawa "Meli Dar Inashusha Mizigo Siku 5, Mombasa Siku 1.25"


Waziri wa Ujenzi Prof. Makame Mbarawa leo June 10,2023 amewasilisha Bungeni maelezo ya awali kuhusu mapendekezo ya kuridhia mkataba baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa Bandari Tanzania ambapo amesema hali ya sasa ya utendaji wa Bandari ya Dar es Salaam imeendelea kuwa ya kiwango cha chini ikilinganishwa na Bandari shindani kikanda, kwa mfano, wastani wa meli kusubiri nangani kwa Bandari ya Dar es salaam ni siku 5 ikilinganishwa na siku 1.25.

“Serikali imeendelea kuwekeza kwenye Bandari zake kwa vipindi tofauti kwa kutumia vyanzo vyake na fedha za mikopo katika kutekeleza mikakati kwa lengo la kuboresha Sekta ya Bandari nchini, mkakati uliochukuliwa hivi karibuni ni utekelezaji wa Mradi mkubwa wa uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam ambao umehusisha uimarishaji na uongezaji wa kina cha gati namba 1-7, ujenzi wa gati jipya la kuhudumia magari na uongezaji wa kina cha lango la kuingia Bandarini”

“Uzoefu umeonesha kuwa uwekezaji wa namna hii una faida kubwa kwa nchi iwapo Bandari itaendeshwa kwa tija na ufanisi mkubwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa, pamoja na kuchukua hatua mbalimbali za maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam, bado ufanisi katika utoaji huduma za Bandari haujafikia viwango vinavyotakiwa Kimataifa”

“Hali ya sasa ya utendaji wa Bandari ya Dar es Salaam imeendelea kuwa ya kiwango cha chini ikilinganishwa na Bandari shindani kikanda, kwa mfano, wastani wa meli kusubiri nangani kwa Bandari ya Dar es salaam ni siku 5 ikilinganishwa na siku 1.25 kwa Bandari ya Mombasa na siku 1.6 kwa Bandari ya Durban”

“Ufanisi mdogo wa Bandari ya Dar es Salaam umetokana na changamoto mbalimbali zikiwemo kukosekana kwa mifumo ya kisasa ya TEHAMA, kutokuwepo kwa maeneo ya kutosha ndani na nje ya bandari kwa ajili ya kuhifadhia shehena pamoja na maegesho ya meli na kukosekana kwa mitambo ya kutosha na ya kisasa ya kuhudumia shehena ambayo teknolojia yake inabadilika mara kwa mara na ina gharama kubwa ya uwekezaji na uendeshaji”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad