'Cha Arusha' Chatajwa Kuwa Bangi Kali zaidi Duniani

'Cha Arusha' Chatajwa Kuwa Bangi Kali zaidi Duniani

Arusha. Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amesema wakati Serikali ikipambana na dawa za kulevya aina ya bangi, aina hiyo ya mmea unaolimwa Arusha ambao ni maarufu kama "Cha Arusha" inatajwa kama ndio bangi kali zaidi duniani .


Bangi hiyo hulimwa na nyingine kujiotea katika viunga vya Mlima Meru na hasa katika Kijiji cha Kisimiri Juu wilayani Arumeru .


Mkuu wa mkoa Arusha, John Mongella ametoa taarifa hiyo leo JunI 25, 2023 katika maadhimisho ya kupinga matumizi ya dawa za kulevya ambayo yanafanyika katika uwanja wa sheikh Amri Abeid.

Mongella amesema kilimo cha bangi kinafanyika katika Kijiji cha Kisimiri Juu kutokana na eneo hilo kuwa na ardhi yenye rutuba kubwa.


"Tumepewa taarifa na wataalam wa dawa za kulevya kuwa bangi ambayo inapatikana Kisimiri ndio bangi kali zaidi duniani na watumiaji wamekuwa wakitumia kwa tahadhari la sivyo inawaharibu," amesema.


Hata hivyo amesema Serikali mkoani Arusha kwa kushirikiana na viongozi wa mila na dini wanaendelea na mkakati wa kudhibiti kilimo cha bangi Kisimiri.


Amesema Serikali kwa miaka imekuwa ikipambana na kilimo cha bangi lakini bado kinaendelea na sasa ndio sababu inashirikisha viongozi wa mila, viongozi wa dini na wananchi.


"Tumeunda kamati ya watu 60 ambayo itapita kwenye mashamba kung'oa bangi kwa kushirikiana na wananchi," amesema.


Amesema elimu inaendelea kutolewa katika Kijiji cha Kisimiri kuachana na kilimo na bangi na kujikita na kilimo cha mazao mengine.


Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo amesema kuanzia machi hadi Juni mwaka huu, tani 615 za bangi zimeteketezwa mkoani Arusha.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad