Davido: Nadondosha chozi kila siku tangu nimpoteze mwanangu

Davido: Nadondosha chozi kila siku tangu nimpoteze mwanangu

Mwanamuziki maarufu Nigeria, David Adekele, anayejulikana na wengi kama Davido amesema kwamba anaendelea kumuomboleza mwanawe Ifeanyi Adekele kila siku.


Davido alizungumza wakati wa mahojiano kwa jina "Million Dollaz Worth of Game."


Anasema kwamba haikuwa rahisi kwake yeye kutoa albamu 'Timeless' baada ya kifo cha mwanawe


Mwanamuziki huyo anasema kwamba anaamini kwamba mama yake na mwanawe wako mbinguni wakifurahia muziki anaofanya na kwamba haruhusu kuvunjika moyo.


‘’Kila siku machozi yanabubujika machoni mwangu kwasababu ya kifo cha mwanagu lakini watu hawajui hilo’’.


‘’Najua kwamba mwanangu ananitazama kutoka mbinguni, mbali na hilo mwanangu hangependa nimvunje moyo kwasababu ya mama yake, lazima niwe mwangalifu kutokana na wapenzi wangu wa muziki kote duniani’’.


Ifeanyi alifariki Oktoba 1, 2022 baada ya kuanguka katika bwawa la kuogelea ndani ya nyumba yao huko Banana Island, Mjini Lagos.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad