Diamond Platnumz na Alikiba Wameridhika?? Kwanini Hawafikii Level za Burna Boy??

Diamond na Alikiba wameridhika?? kwanini hawafikii level za Burna Boy??

Kupitia kipindi cha RECAP & MANDO @el_mando_tz ameeleza namna nafasi za wasanii wakubwa kama Diamond na Alikiba walivyo na nnafasi kubwa ya kuliwakilisha taifa kwenye tuzo kubwa na matamasha makubwa zaidi duniani akitolea mfano BET ambapo Burna boy alichukua tuzo na Davido kutoa burudani.

Anaeleza kuwa kuna namna wasanii wetu wa Tanzania wameridhika kutokana na mafanikio waliyokuwa nayo ya kimuziki, huenda malengo yao ya kimaisha ambayo walikuwa wanataka kuyafikia wameshayafikia tayari.

Ukiangalia namna wanavyofanya muziki kwa sasa unaona kabisa wamesharidhika na maisha yao ya sasa.

@el_mando_tz anauliza kuwa kwanini wasanii wetu ni wepesi sana kuridhika?? kimafanikio ukiangalia mafanikio ya wasanii wa Nigeria mfano Burna boy, Davido, Wizkid na wengine unaona kabisa bado wana njaa kimafanikio na wanataka kufika mbali.

Kwanini wao hawaridhiki haraka kama wasanii wetu?? unahisi wasanii wetu tatizo liko wapi??

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad