DJ Brownskin Aliyemrekodi Mkewe Akinywa Sumu na Kujiua Bila Kumsaidia Aachiwa Huru


Michael Macharia Njiiri maarufu kama DJ Brownskin, ameachiwa kwa dhamana ya KSh. 200,000 zaidi ya TSh. Milioni 3 baada ya kukaa kizuizini kutokana na tuhuma za kusaidia kifo cha mkewe kilichotokea mwaka jana.

Siku ya Jumatatu, Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Milimani, Lukas Onyina alisema kwamba hakukuwa na sababu zinazowalazimisha kuendelea kuwa kizuizini na kutoa agizo la kumwachilia DJ Brownskin kwa dhamana.

"Nimezingatia ripoti iliyoko mbele yangu ambayo inampa faidi mshtakiwa kwamba hana hatari ya kukimbia ikiwa ataachiliwa. Nampa dhamana ya KSh. 200,000 au dhamana ya fedha taslimu ya KSh. 100,000".

Onyina aliagiza kuwa kesi hiyo itasikilizwa tena Mahakamani Juni 22.

Dj Brownskin, ambaye amekuwa rumande kwa siku 14, alishtakiwa kwa mashtaka matatu ambayo ni kusaidia kujitoa uhai, kupuuza kuzuia uhalifu na kuharibu ushahidi kwa kufuta video alizo-post kwenye mtandao wake wa kijamii kuhusiana na kisa cha kujiua cha mkewe Sharon Njeri nyumbani kwao mnamo Julai 29, 2022.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad