Eng. Hersi "Naamini ‘CAF’ itaiadhibu klabu ya USMA Kwa Vurugu Walizotufanyia" "


Rais wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans Injinia Hersi Said anaamini Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ litaiadhibu klabu ya USMA, kwa vitendo vya kukiuka taratibu za mchezo ambao upo chini ya Shirikisho hilo.

Juzi Jumamosi (Juni 03) Mashabiki wa USMA waliwasha Fataki kwa nyakati tofauti uwanjani hali ambayo ilisababisha mchezo wao dhidi ya Young Africans kusimamishwa na mwamuzi kutoka nchini Mauritania Dahane Beida.

Akizungumza mapema leo Jumatatu (Juni 05), katika mahojiano na Kituo cha Wasafi FM, Injinia Hersi Said amesema ‘CAF’ wamekuwa wakali sana kwa timu ambayo huonekana kuwa chanzo cha kuharibu taratibu za mchezo, huku akikumbushia adhabu iliyowahi kuikuta klabu yake na kupelekea kutozwa faini ya Dola za Marekani Elfu 35.

“Sisi Young Africans tulipigwa Faini ya Dolla Elfu 35 kwa sababu ya moshi uwanjani. USM Alger juzi kipindi Djuma Shabani anaenda kupiga Penati wamepiga fataki nyingi sana kama zile za kukaribisha mwaka Mpya.”

“Lile ni kosa na wataadhibiwa, lakini walifanya vile Purposely kwa makusudi Kwa sababu walikua wanataka Ubingwa hivyo wala hawajali” amesema Injiani Hersi

Katika mchezo huo Young Africans ilishinda 1-0, lakini ilishindwa kutwaa Ubingwa wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika kufuatia sheria ya bao la ugenini kuibeba USMA iliyoshinda 2-1 katika mchezo wa Mkondo wa Kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam Jumapili (Mei 28).

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad