Tulipofika sasa hivi ni lazima tujue kutofautisha urafiki na kazi, lazima kuwe na weledi ili kuzuia mikingamo na ugomvi.
Ukifatilia sakata la Feitoto utagundua hakukuwa na weledi kuanzia awali kabisa badala yake ilikuwa ni jambo la mahusiano.
Ndio maana leo hii Feisal analalamika kunyanyaswa na mtu lakini sio taasisi. Hili inaonekana ni jambo la watu wawili ambao wameshindwa kuelewana.
Kama wote wawili walipaswa kutofautisha kazi na mambo/mahusiano binafsi, kiongozi wa taasisi angemhudumia mchezaji kama mfanyakazi wa taasisi sio kama washkaji.
Kuna wakati kiongozi na mfanyakazi wanaishi kama marafiki lakini wakati wa kazi lazima kila mmoja abaki katika nafasi yake. Kwa hiyo kiongozi alipaswa kujua wakati gani anaiwakilisha taasisi kwenye kazi na wakati gani wa ushkaji.
Ukifatilia sakata zima unaona kuna mapungufu mengi yamejitokeza, sisi kama wadau ambao jambo hili linatuhusu huu ndio wakati wa kufanya mageuzi ya namna gani tunavyofanya vitu vyetu.