Mayele na Kocha Nabi |
Bosi huyo wa Young Africans SC alitoa taarifa kwa kikosi chake wikendi hii kabla ya parade la Ubingwa kuwa atawaacha Wananchi mwishoni mwa kandarasi yake.
Baada ya kukataa pendekezo la kuongezewa mkataba wa miaka miwili mipya, kocha huyo wa Tunisia anatafuta changamoto mpya katika maisha yake ya soka baada ya kushinda mataji matatu ya nyumbani msimu huu na kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF.
Kaizer Chiefs kwa mara ya kwanza waliongea na kocha Nabi takribani wiki mbili zilizopita, na baada mazungumzo ya awali, pande zote mbili zilikubali kuwa wasubiri mchezo wa fainali ya FA upite ndipo waanze kuzungumzia maslahi binafsi.
Awali Nabi alipokea ofa nzuri kutoka kwa Raja Club Athletic, Wydad Athletic Club na Esperance katika miezi ya hivi karibuni lakini akakataa ombi lao la kutaka kuondoka Yanga katika kipindi ambacho ligi zilikua hazijaisha na bado walikuwa wanawania vikombe viwili.
Nabi amewapa masharti Kaizer Chiefs ya kwenda na kocha wake msaidizi, kocha wa makipa, na kocha wa viungo, iwapo atateuliwa kuwa kiongozi wa kuinoa miamba hiyo ya Soweto msimu ujao.
Ikiwa Kaizer Chiefs watakuwa tayari kukubali masharti au kuingia kwenye mazungumzo zaidi, bosi huyo wa zamani wa Al-Merrikh SC anaweza kuwasili mapema wiki ijayo kuhitimisha hatua hiyo lakini kwa jinsi mambo yalivyo, ni kugusa na kwenda.
Kwenye dili hili huenda kocha Nasredine nabi akaondoka na Fiston Mayele ambaye pia Kaizer Chiefs wameonyesha nia ya kumtaka.