Hali ya wasiwasi yatanda Moscow, Putin hajulikani aliko




Hali ya wasiwasi yatanda katika mji wa mkuu wa Urusi, Moscow. 
Hayo yanajiri wakati kuna uvumi unaosambaa Moscow kuhusu kutoroka kwa Vladimir Putin katika mji huo.


"Rais anafanya kazi Kremlin," anasema msemaji wake Dmitry Peskov, aliyenukuliwa na shirika la habari la serikali la Ria Novosti, ambalo lilimuuliza kuhusu uvumi unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii unaodai kwamba rais Putin aliondoka Moscow kwa sababu ya uasi wa kundi la Wagner.

Wakazi wa jimbo la Lipetsk watakiwa kusalia nyumbani

"Ili kuhakikisha utaratibu na usalama wa raia wa jimbo la Lipetsk, Halmashauri ya kikanda inatoa wito kwa wakazi wasiondoke manyumbani kwao isipokuwa kama kuna ulazima, na kukataa kusafiri kwa magari ya kibinafsi" , imebaini akaunti ya Telegram ya mamlaka ya jimbo hilo,  linalopatikana kilomita 420 kusini mwa Moscow. Wito huu unaambatana na matangazo kwenye Twitter ya video zinazoonyesha safu ya magari, baadhi yao yakiwa yamebeba mizinga, yakipita kwenye barabara ya shirikisho ya M4 kwenye eneo laa mji wa Horse-Kolodezsky, katika jimbo la Lipetsk.


Ripota wa shirika la habari la Reuters anaripoti kuona msafara magari ya wapiganaji wa Wagner wakisafiri kutoka kusini mwa Urusi kuelekea Moscow, wakipita mji wa Voronezh. Angalau gari moja inabeba kifaru cha kijeshi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad