Tanzania kama nchi kwa msimu wa 2022/23 tulimaliza na pointi 56.5 nafasi ya 6 kwenye Association Ranking nyuma ya mataifa 5 (Morocco, Misri, Algeria, Afrika Kusini na Tunisia) na kufanikiwa kuwa mojawapo ya mataifa 12 ambayo yatawakilishwa na timu 4 kwenye mashindano ya CAF msimu 2023/24 ikiwa timu 2 (Yanga na Simba) kwenye klabu bingwa Afrika na timu 2 (Azam na Singida) kwenye kombe la shirikisho.
Katika pointi 56.5 za msimu 2022/23 zimepatikana kwa kufanya vizuri kwa timu 3 (Simba, Yanga na Namungo) kwa misimu mitano ya mashindano tangu msimu wa 2018/19 hadi 2022/23 katika misimu hiyo Simba imekusanya jumla ya pointi 35, Yanga imekusanya jumla ya pointi 20 na Namungo imekusanya jumla ya pointi 1.5 ukilijumlisha (35+20+1.5) utapata jumla ya pointi 56.5
Kutoka msimu mmoja kwenda msimu mwingine pointi za timu na nchi husika huwa zinapungua, kwa msimu wa 2023/24 pointi za Tanzania ni 41 ikiwa zimepungua pointi 15.5 kutoka pointi 56.5 Ila Tanzania kama nchi bado tupo nafasi ya 6 nyuma ya mataifa matano yale yale. Msimu 2023/24 tunaanza pointi zetu 41 ambazo zimepatikana kutoka timu 3 za Tanzania Simba (24), Yanga (16) na Namungo (1) kwa hesabu ya misimu mitano ya kuanzia msimu 2019/20 hadi 2023/24.
Kwenye Club Ranking ya msimu 2023/24 Simba imepanda kutoka nafasi ya 9 hadi nafasi ya 7 nyuma ya vilabu (Al Ahly, Wydad, Esperance, Raja, Mamelodi na CR Belouzdad) ikiwa na pointi 24 sawa na vilabu vya Pyramid ya Misri na Petro de Luanda vikiwa na pointi 24 pia Yanga kwenye Club Ranking ya msimu 2023/24 imepanda kutoka nafasi ya 18 hadi nafasi ya 16 ikiwa na pointi 16 sawa na Orando Pirates ya Afrika Kusini.
Msimu 2023/24 umeandikiwa pointi 0 kwa kila timu au nchi ambazo ndio zinaenda kutafutwa kwa msimu husika na pointi zinaanza kuhesabiwa iwapo timu itafanikiwa kuingia kwenye hatua ya makundi.