Idadi ya Wachezaji Wakubwa Wanaokimbilia Saudi Arabia Yaongezeka, Ligi Kuu ya England kuzuia uhamisho


Mchambuzi wa soka, Gary Neville ametoa wito kwa Ligi Kuu ya England kuzuia uhamisho wa wachezaji kwenda Saudi Arabia.

Gary Neville amewaambia BBC Sports kwamba “Premier League inapaswa kuweka vikwazo mara moja kwa uhamisho kwenda Saudi Arabia ili kuhakikisha uadilifu wa mchezo hauharibiki. Uchunguzi ufanywe kuhakikisha uhalali wa hamisho hizo.

“Ninaamini, kwa sasa, usajili unapaswa kusimamishwa na kuchunguza muundo wa umiliki wa Chelsea ili kuona kama kuna mikataba ya uhamisho yenye manufaa kwa klabu hiyo ambayo si sahihi.”

Idadi ya wachezaji wanaoelekea nchini Saudi Arabia imeongezeka maradufu, na kushudia wachezaji kama nahodha wa Wolves Ruben Neves, Kalidou Koulibaly, Hakim Ziyech Pamoja na Edouard Mendy ambao bado wako kwenye kiwango bora wakielekea nchini humo.

Saudi Arabia pia imeshuhudia uhamisho wa wachezaji walio karibu na kumaliza ungwe ya maisha yao ya soka kama Christiano Ronaldo, N'golo Kante pamoja na Karim Benzema waliotimkia nchini humo huku Lionel Messi akiikataa ofa kubwa kutoka Al Hilal ili kujiunga na Inter Miami ya Marekani

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad