Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), imeujulisha Umma kuwa, Vijana waliomaliza kidato cha sita na kuchaguliwa kujiunga mafunzo kwa mujibu wa sheria kwa mwaka huu na walishindwa kuripoti kwa muda waliopangiwa hawatapokelewa makambini hivyo wasiende kuripoti.
kauli hiyo imesemwa na Brigedia Jenerali Hassan Mabena, Mkuu wa Tawi la Utawala JKT akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam
Brigedia jenerali Mabena ameongeza kuwa vijana wote waliochaguliwa walitakiwa kufika katika kambi walizopangiwa kuanzia tarehe moja mpaka 11 mwezi wa sita lakini baadhi ya vijana hao hakuweza kuripoti na badala yake sasa ndio wanaenda kuripoti kinyume na utartibu waliopewa na kuchelewesha kuanza kwa masomo hivyo sasa jeshi limesitisha ili kuruhusu vijana waliopo makambini kuendelea na masomo.