Kifaa cha Kwanza Cha Yanga Utaambulisho Wake Waandaliwa Maalum Usipime


IMEBAINIKA kuwa, kuna chuma kipya Yanga kipo mjini tayari na huenda kikatambulishwa kupitia mkutano mkuu wa klabu hiyo unaotarajiwa kufanyika keshokutwa Jumamosi katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar Es Salaam.

Katika mkutano mkuu wa mwisho kufanyika mwaka jana ambao ulikuwa na ajenda pia ya uchaguzi mkuu ambapo alipatakana mshindi ambaye ni rais wa sasa wa Yanga Injinia Hersi Said, mashabiki wa Yanga walipewa sapraizi.

Hersi baada ya kutangazwa kuwa Rais wa Yanga, alimtambulisha aliyekuwa kiungo wa Newcastle United ya England, Gael Bigirimana na kuibua shangwe zito japo usajili huo haukulipa ndani ya Yanga.

Tayari chanzo chetu makini kutoka Yanga, kimelipa Spoti Xtra taarifa za uhakika juu ya uongozi wa Yanga huenda ukawapa sapraizi nyingine ya usajili wa mchezaji huku pia kukiwa na taarifa za Yanga kumshusha mmoja ya wachezaji ambaye tayari kila kitu wamemaliza na kumtambulisha siku hiyo ya uchaguzi mkuu.

“Yanga kwenye mkutano huu mkuu huenda wakamshusha mchezaji wa maana na kumtambulisha kama ambavyo walifanya kwa Gael Bigirimana msimu uliopita ambapo walimtambulisha kupitia mkutano mkuu.

“Kama ambavyo unafahamu kuwa kwa sasa ndani ya Yanga kuna mambo mengi yanaendelea haswa kwa wachezaji wanaoachwa na wale walioondoka kama Kocha Mkuu Nasreddine Nabi na kocha wa makipa Milton Nienov.

“Hivyo kwa wale watakaoingia huenda kupitia mkutano mkuu akatambulishwa mchezaji mmoja kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wananchi wanapata amani juu ya usajili wa msimu huu,” kilisema chanzo hicho.

STORI NA MARCO MZUMBE

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad