Kimenuka...Mashabiki Kaizer Chiefs Hawamtaki Kocha Mpya Waliomtangaza na Kumuacha Nabi



Ni kama mashabiki wa klabu inayoshiriki Ligi Kuu nchini Afrika Kusini hawajaridhishwa na usajili wa kocha wao mpya Molefi Ntseki aliyetambulishwa hapo jana.

Mkufunzi huyo wa zamani wa Bafana, baada ya kutangazwa kuwa kocha mkuu mpya wa Kaizer Chiefs mashabiki wa klabu hiyo walimiminika kwenye sehemu ya comments na kutoa maoni yao ambayo yanaonesha kuto kuunga mkono ujio wa kocha huyo.

Matarajio ya wengi ilikuwa huwenda aliyekuwa kocha wa klabu ya Yanga Mtunisia, Nasreddine Nabi angetambulishwa ila imekuwa tofauti huku taarifa zikieleza kuwa dili la Profesa Nabi kutua AmaKhosi liliota mbawa dakika za mwisho.

Kocha Nabi na viongozi wa Kaizer Chiefs walishindwana kwenye kipengele cha kutaka kuingia na benchi lake la ufundi analolitaka kitendo ambacho viongozi wameshindwa kuafikiana sababu zikitajwa ni gharama kubwa.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad