Kipimo Cha Mimba Chaonesha Mwanaume ni Mjamzito


Kwa mujibu wa Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mwaka 2021/ 2022 imebainika kuwepo kwa Mazingira yasiyofaa ya kuhifadhia dawa na vifaa tiba wa katika baadhi ya hospitali na vituo vya afya hali iliyopelekea baadhi ya dawa pamoja na vitendanishi kuharibika kabla ya muda wake na kutoa majibu yasiyo na usahihi

Hayo yameelezwa Ikulu Zanzibar na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Zanzibar Dkt. Othman Abbas Ali ambapo amesema Baadhi ya vituo vya afya na Hospitali vililazimika Kusitisha vipimo vya upimaji wa mkojo kwaajili ya ujauzito (UPT) baada ya kuonekana Vinatoa majibu tofauti ikiwa ni pamoja na Kipimo hicho Kuonesha Mwanaume ana ujauzito

"Mhe. Rais Dkt. Mwinyi Tumekwenda vituo vya afya ukienda pale Ukiwa Mjamzito tumbo kubwa unaonekana si Mjamzito na ukiwa si Mjamzito ukienda unaonekana ni Mjamzito Sitaki kuvitaja hapa

"Lakini pia Kulifanyika kipimo cha mkojo kilibaini Mwanaume pia ni Mjamzito" - Dkt. Othman Abbas Ali, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Zanzibar alipokuwa akiwasilisha Taarifa za Ukaguzi wa Hesabu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar leo Juni 3, 2023.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad