Kisa Fei Toto Kwenda Azam FC, Mayele Avunja Ukimyaaaa..Aweka Wazi Yaliyoko Moyoni

 

Kisa Fei Toto Kwenda Azam FC, Mayele Avunja Ukimyaaaa..Aweka Wazi Yaliyoko Moyoni

Zikiwa zimepita saa chache tangu kutangazwa rasmi kwa mchezaji Feisal Salum kujiunga na Azam FC.

Mshambuliaji wa Yanga Raia wa Congo, Fiston Mayele ambae amekipiga na mchezaji huyo katika Klabu ya Yanga ametoa neno kwa mchezaji huyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram mayele ameweka Picha akiwa na Feisal pamoja na Video alimtengenezea pasi ya bao na kuandika;

“kila heri fundi mpira kwa majikumu yako mpya mwanangu”

Nae Feisal alirudi katika Commeny na kumjibu mayele;

“Asante sana bro”

Feisal amejiunga na Yanga mpaka mwaka 2026 huku bei aliyouzwa ikiwa haijawekwa wazi.

Feisal Salim ‘Fei Toto’ amejiunga Azam FC kwa mkataba wa miaka mitatu , ambapo Yanga wamelipwa Tsh Mil 270 kukubali kufanya biashara hiyo.

Duru kutoka ndani ya klabu ya Azam FC zinasema kuwa, Fei Toto atakuwa akilipwa Milioni 16 kwa mwezi ikiwa niongozeko mara nne  kutoka mshahara wa Milioni 4 aliokuwa akilipwa Yanga.

Mbali na mshahara huo, Fei Toto pia atapatiwa Nyumba ya kisasa, gari kali ya kutembelea pamoja na kuhakikishiwa namba kwenye kikosi cha kwanza cha matajiri hao wa Chamazi.

Kuelekea msimu ujao, Azam FC wamejipanga kufanya kweli, ambapo wameanza kuboresha sehemu mbalimbali kwenye kikosi chao ikiwemo kumpa mkataba kocha Msenegali.

Hii inakuja ikiwa tayari wanauhakika wa kushiriki mashindano ya kimataifa Mwakani, ambapo kuna uwezekano wakashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika endapo watashinda kombe la Shirikisho la ASFC ambapo bingwa wake anashiriki Ligi ya Mabingwa pamoja na Bingwa wa Ligi Kuu.

Hata hivyo, ikitokea wakapoteza mchezo huo mbele ya Yanga, basi watashiriki kombe la shirikisho Afrika kwa kigezo cha kumaliza ligi nafasi ya tatu kwenye msimamo.

Timu zingine zenye uhakika wa kushiriki mashindano ya CAF msimu ujao ukiachana na Yanga ambao tayari wanauhakika wa Ligi ya Mabingwa, ni pamoja na Simba SC ambao hatma yao inategemeana na matokeo ya Fainal ya Kombe la shirkiriko la ASFC ili kujua endapo watashiriki Ligi ya Mabingwa au kombe la shirikisjo endapo Azam FC watafungwa au kushinda kombe hilo.

Timu nyingine ni Singida Big Stars ambao yenyewe itashiriki Kombe la Shirikisho Afrika, kutokana na kumaliza ligi kwenye nafasi ya nne.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad