Kiungo Nelson Okwa Aendelea Kuivua Nguo Simba "Hawajanilipa Pesa za Kuvunja Mkataba"

Kiungo Nelson Okwa Aendelea Kuivua Nguo Simba "Hawajanilipa Pesa za Kuvunja Mkataba"
Nelson Okwa

Licha ya kuoneshwa mlango wa kutokea katika Kikosi cha Simba SC, Kiungo Nelson Okwa amelalamika kutolipwa stahiki zake mara baada ya kuvunjiwa Mkataba na Klabu ya Simba.

Akizungumza kwa mara ya kwanza tangu apewe "Thank You" Okwa anasema;

“Baada ya kuvunja mkataba walisema watanilipa pesa ya kuvunja mkataba lakini bado hadi sasa sijapokea chochote, lakini wamesema wapo kwenye mchakato wa kunilipa, kwa sasa wanipe tiketi ya ndege niondoke nikifika Nigeria kama watanilipa ni sawa,”

Okwa alibakisha Mkataba wa mwaka Mmoja na Klabu ya Simba na muda mwingi alikuwa kwa Mkopo katika Timu ya Ihefu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad