Kocha Juma Mwambusi Atoa Machozi Mbeya City Kushuka Daraja "Madiwani Walikuwa Wanaingilia Kazi ya Kocha"

Kocha Juma Mwambusi Atoa Machozi Mbeya City Kushuka Daraja "Madiwani Walikuwa Wanaingilia Kazi ya Kocha"


Kocha Juma Mwambusi ambaye aliipandisha Ligi Kuu timu ya Mbeya City, amesema amesikitishwa na timu hiyo kushuka daraja huku akisema uongozi mbovu ndio sababu ya Mbeya City kushindwa kubaki Ligi Kuu.

Mwambusi amesema kuna wakati Madiwani walikuwa wanaingilia mambo ya kiufundi wakati hawana taaluma nayo!

“Ni majonzi mazito! Huwezi kuitaja Mbeya City bila kumtaja Juma Mwambusi, ni sehemu ya maisha na CV yangu kwa wakati ule tunapambana kuipandisha.

“Tulimwaga jasho na Mkurugenzi wa wakati ule Juma Idd na uongozi wake shupavu lakini watu walikuwa hawaingilii shughuli za kiufundi wakati wa mapambano yote.

“Ni masikitiko timu imeshuka lakini bado hata kiutawala kulikuwa kuna shida kwa sababu kuna wakati timu ilikuwa inafanya vibaya nikarudi kwenda kujaribu kusaidia lakini nikichokutananacho niliamua kuondoka haraka kabla sijashusha heshima yangu.

“Kama madiwani wanaingilia kazi za kiufundi za timu, ni fani ambayo hawana ujuzi nayo kwa hiyo hata angakuja Kocha kutoka wapi nilikuwa naona ugumu wa Mbeya City kufanya vizuri.

“Badala yake zinakuja hamasa wakati mambo yameshakuwa magumu, haiwezekani. Kila kitu kinakuwa na maandalizi yake mapema.

“Ni masikitiko makubwa sana kuipoteza Mbeya City, ni timu kubwa ambayo imeweza kujitangaza na kuutangaza mkoa wetu wa Mbeya,” amesema Mwambusi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad