Kocha Robertinho: Timu Nyingi Zinanitaka

Kocha Robertinho: Timu Nyingi Zinanitaka


Kocha Mkuu wa Simba,Robert Oliveira 'Robertinho'amewahakikishia mashabiki kwamba kuna mapinduzi makubwa yanakuja kwenye usajili wa klabu hiyo.


Robertinho amesema kuwa ameshakutana na mabosi wa juu wa klabu yake na kutengeneza mikakati ya kukisuka kikosi chao na ameridhika na makubaliano yao kwamba mastaa watakaokuja watakuja kuwarudishia hadhi iliyopotea kwenye mataji.


"Kitu ambacho kipo mbele yetu sasa kwanza ni kumalizia hizi mechi mbili za mwisho za ligi Mimi ni kocha ninayetaka kushinda kila wakati na hiki ndicho pia mashabiki wa Simba wanastahili,"alisema Kocha huyo ambaye kwa uchache anataka wachezaji 10 wapya.


"Tutakapomaliza msimu wapo wachezaji tutaachana nao kwa heshima lakini vikao vyangu na viongozi wangu wa klabu tutakwenda kuleta wachezaji bora ambao watarudisha heshima yetu ili tuwe kwenye eneo ambalo tunastahili.


"Tutaleta wachezaji ambao wana njaa ya mafanikio kwa hadhi ya Simba na sio vinginevyo,Simba ni klabu ya makombe sio kuwa hapa tulipo,"alisema Kocha huyo ambaye Mwanaspoti linajua ameshamalizana na Moses Phiri na atasalia Msimbazi kukiwasha msimu ujao.


Ni msimu wa pili sasa Simba imekosa mataji ambao yamekuwa yakitua kwa watani wao Yanga ambao wako kwenye ubora wao na sasa Robertinho amewatumia salamu Jangwani kwamba kuna mziki unakuja.


Amewataka wale mashabiki wa Simba watulie wakati huu wanakwenda kumalizia mechi mbili za mwisho za ligi kisha kazi ya kushusha vifaa itaanza na wamejipanga tofauti na misimu iliyopita kwani watafanya kitaalam zaidi kwavile levo waliyofikia ni kubwa kwa sasa.


Raia huyo wa Brazil, aliongeza kuwa ameachana ofa nyingi kutoka maeneo mbalimbali baada ya kuridhika na malengo ya Simba kwa msimu ujao haswa kimataifa na uongozi umemwambia atulie.


"Ilikuwa presha kubwa kwangu, ofa zilikuwa nyingi lakini nimeamua kubaki hapa nawapenda mashabiki wa Simba lakini kubwa hata viongozi wamekuwa wakinipa ushirikiano mkubwa, nafurahia mpango mzuri kuelekea msimu ujao,"alisema Kocha huyo ambaye amepania kila nafasi msimu ujao iwe na vifaa viwili bandika bandua.


Inafahamika kwamba, Augustine Okra, Nelson Okwa, Ismael Sawadogo na Gadiel Michael ni wachezaji ambao kwa kuanzia watang'oka Msimbazi na muda wowote watapewa barua zao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad