Kuchomwa kwa Quran, Balozi arudishwa




Morocco imemrudisha nyumbani Balozi wake nchini Sweden kufuatia kuchomwa kwa Quran takatifu kwenye maandamano Mjini Stockholm.

Vyombo mbalimbali vya Habari nchini Morocco vimeripoti kwamba Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Morocco imekitaja kitendo hicho kuwa cha kuudhi na kutowajibika katika wakati ambapo Waislamu walikuwa wakisherehekea mojawapo ya siku takatifu zaidi katika kalenda yao.

Mratibu wa maandamano hayo ambaye anasemekana kuwa Mzaliwa wa Iraq Salwan Momik – anachunguzwa kwa uchochezi wa chuki.

Mahakama ya Sweden iliamua maandamano hayo yaruhusiwe kuendelea kwa misingi ya uhuru wa kujieleza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad