Luc Eymael Aishika Pabaya Yanga, Kutupwa nje Michuano ya CAF


  

Yanga wanaweza kukumbana na rungu la kufungiwa kusajili madirisha matatu ya usajili pamoja na kuondolewa kwenye Michuano ya Kimataifa msimu ujao.


Eymael aliiburuza Yanga kwa Shirikisho la Kimataifa la Soka Duniani (FIFA) kwa kosa la kuchelewa kumlipa madai yake miezi michache baada ya kibarua chake kuota nyasi, Septemba 2021. Hata hivyo, Yanga ilikubali kumlipa kocha huyo kwa awamu.


Kwa mujibu wa notisi ya malipo ya Eymael, Yanga ilipaswa kumalizana naye ndani ya siku 45 huku kuanzia Juni 9 mwaka huu ikitakiwa kulipa na riba ya asilimia tano hadi juzi Ijumaa ambapo ilikuwa siku ya mwisho kumaliza deni la Dola 66,000 sawa na Sh. 157milioni.


Kocha huyo, amefunga kupitia kituo cha SABC kuwa asilaumiwe kwa kile ambacho FIFA inaweza kufanya kufuatia Yanga kushindwa kukamilisha walikubaliana kuhusu malipo yake kwani hadi siku ya mwisho, juzi walikuwa wamemlipa nusu ya kiwango.


“Nimekuwa nikifanya nao mawasiliano lakini naona wamekuwa kimya, kwa kuwa hili suala limefika kwenye mamlaka husika kwa hiyo tutaona kile ambacho wataamua, wanaweza pia kuingia kwenye adhabu ya kupokonywa pointi tisa. Mwaka 2018 au 2017, Amazulu ilikuwa na kesi kama hii, haikulipa, hivyo FIFA iliilazimisha kulipa au kushuka daraja kabla ya msimu mpya kuanza, siku zote hakuna aliye juu ya sheria,” alisema kocha huyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad