Kazi za Ualimu |
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imewaita kazini walimu 13,130 kwa ajili ya kufundisha wanafunzi katika ngazi ya shule za msingi na sekondari.
Orodha ya Waombaji ajira iliyochapishwa leo Juni 5, 2023 katika kurasa 515 imehusisha walimu ambao pia wamesoma na kuhitimu elimu maalum.
Waziri wa Tamisemi, Angellah Kairuki amesema Waajiriwa wapya ambao hawataripoti katika vituo walivyopangiwa ndani ya siku 14 kuanzia tarehe ya tangazo hili, watakuwa wamepoteza nafasi zao na nafasi hizo zitajazwa na waombaji wengine wenye sifa waliopo kwenye Kanzidata (Database) ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI.
Mwezi Aprili, 2023 Rais Samia Suluhu Hassan, alitoa kibali cha ajira ya watumishi 21,200 kati yao 13,130 walikuwa wa kada ya Ualimu na 8,070 wa kada za Afya.