The Best Rapper Alive, Dwayne Michael Carter Jr maarufu Lil Wayne amesema hawezi kukumbuka hata nyimbo zake mwenyewe kutokana na kupoteza kumbukumbu.
Alipoulizwa na Rolling Stone mapema mwezi huu (Juni) jinsi anavyochukulia albamu yake ya "Tha Carter III" miaka 15 baadae, rapper huyo alikuwa mkweli kwa kusema;
"Nitakuwa wazi kabisa, Sijui chochote kuhusu Tha Carter III, Tha Carter II, Tha Carter One au hata Tha Carter IV. Na huo ndio ukweli wangu wa Mungu".
"Unaweza kunidanganya, unaweza kunieleza kuhusu nyimbo fulani, hata sitajua tunazungumzia nini. Kwa hiyo, haina umuhimu wowote kwangu kabisa".
"Nina amini kwamba [Mungu] amenijaalia akili hii ya ajabu, lakini hakunikirimu kumbukumbu ya ajabu ya kukumbuka mambo ya ajabu kama haya".
Rapper wa "A Milli" ana historia ya kushikwa na mshtuko wa kifafa na aliweka wazi mwenyewe kuwa ana ugonjwa wa huo mwaka 2013.
Mwezi Februari 2022, ndege yake ililazimika kutua kwa dharura huko Omaha, Nebraska, baada ya kupata mshtuko "mdogo" wa kifafa mara mbili, kwa mujibu wa wawakilishi wake.
Ripoti zinaeleza kwamba alikuwa na mshtuko wa kifafa mwaka 2017, 2016 na 2013 ingawa hiyo labda sio matukio pekee.
"Nimepata mshtuko wa kifafa mara nyingi, nyote tu hamsikii kuhusu hivyo," - kauli ya mwaka 2013.
Licha ya vitisho vya afya, Wayne anasema hana nia ya kustaafu kufanya muziki kamwe.
"Wakati wewe ni msanii - msanii wa kweli kama mimi, nilizaliwa hivi," "Wasanii wa kweli na wapenzi, hawastaafu kamwe. Wanaendelea kufanya hivi hadi wanapofariki."