Tangu mwanzoni mwa miaka ya 2000, mastaa wa muziki nchini Nigeria wamekuwa wakizifuata njia ya mafanikio na kufikia mafanikio ya kuvutia ambayo yameipeleka Afrobeats kwa wasikilizaji wa Kimataifa.
Wakali wa Nigeria wamefanikiwa kushinda tuzo za kimataifa za hadhi ya Dunia, kwa mafanikio yao makubwa na mchango usioweza kupimika katika kuhamasisha muziki wa Nigeria.
Afrobeats ina historia ndefu ya nyota mashuhuri kimataifa, kutoka kwa mafanikio ya makubwa yaliyofikiwa na 2Baba, D'banj, na P-Square katika miaka ya 2000 hadi mafanikio makubwa yaliyofikiwa na Wizkid, Davido, Ice Prince, Tiwa Savage, na Yemi Alade, na mafanikio zaidi ya hivi karibuni ya Burna Boy, Rema, Tems, CKay, na Ayra Starr.
Hapa kuna wasanii 10 wa Afrobeats ambao wameshinda tuzo za kimataifa.
Wizkid Wizkid ndiye staa anayeongoza katika Afrobeats ya siku za hivi karibuni na pia ameshinda tuzo za kimataifa za Grammys, Billboards Awards, Mobo Awards, BMI London Awards, na BET Awards.
Davido Davido ni msanii mwenye wafuasi wengi zaidi barani Afrika na moja ya wasanii wakubwa duniani. Ameshinda tuzo za kimataifa ikiwa BET Award, MAMA Awards, Channel O, na KORA.
Burna Boy African Giant ametajwa kwenye vipengele mbalimbali vya tuzo za kimataifa za muziki. Ametokea kama mshindi katika baadhi tuzo hizo kama vile Festival, BET Awards, Grammy Awards, MTV Europe Music Awards, na Mobo Awards.
Tems Tems alijipatia umaarufu katika tasnia ya muziki mwaka 2020 baada ya kushiriki katika wimbo wa Wizkid uitwao "Essence". Ameshinda tuzo za kimataifa kama vile BMI London Awards, Soul Train Music Awards, BET Awards, Academy Awards, NACP Image Awards, na Silver Clef Awards.
Yemi Alade Yemi Alade mwenye mvuto ameunganisha wasikilizaji barani Afrika na muziki wake mzuri. Mafanikio yake makubwa katikati ya miaka ya 2010 yalimfanya ashinde tuzo ya MAMA kwa kipengele cha Best Female mwaka 2015 na 2016.
D’banj Katika kilele cha uwezo wake, mtayarishaji wa nyimbo mkali alitawala mandhari ya muziki wa Afrobeats na tasnia ya muziki ya Kiafrika. Wakati huo, alishinda tuzo kadhaa za kimataifa ikiwa ni pamoja na BET mwaka 2011.