Mayele amkosha Kochampya Young Africans








Inaelezwa kuwa Uongozi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans una majina mawili ya makocha waliopitishwa kwenye mchujo wa kukinoa kikosi cha klabu hiyo, wa kwanza ni Jozef Vukusic raia wa Slovakia na wa pili ni raia wa Morocco ambaye jina lake limefichwa huku mmoja wao akimkubali Fiston Mayele.

Kamati ya Utendaji na Mashindano ya Young Africans ilikutana kwa ajili ya kukamilisha mchakato wa kumpata kocha mkuu wa timu hiyo baada ya Mtunisia Nasreddine Nabi kumaliza mkataba wake na kusepa.

Kocha Vukusic ambaye ana leseni ya UEFA Pro anayehusudu mfumo wa 4:3:3 amewahi kuzifundisha klabu nyingi Afrika ikiwemo Polokwane na Amazulu zote za Afrika Kusini na mara ya mwisho ameinoa Kosice hadi mwaka jana.

Chanzo cha habari kutoka Young Africans kimeeleza kuwa, kabla ya Vukusic mwenye umri wa miaka 58, kutua klabuni hapo aliomba kutumiwa kikosi kizima na sasa amekipangua kwa kumkataa Tuisila Kisinda ambaye ameshasepa, huku akimsifia Bernard Morrison.


“Hadi sasa kuna CV za makocha wawili ambaye mmoja ni raia wa Morocco na mwingine ni huyu Msolvakia. Hao wote walitumiwa kikosi chetu na kila mmoja ametoa mapendekezo yake mmoja akimtaka Mayele abaki na mwingine akimsifia Morrison.

“Bila shaka kama kamati itapiga kura ya mwisho basi kuna uwezekano mkubwa ndani ya siku hizi mbili atatambulishwa na atatua rasmi kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao,” kimeeleza chanzo hicho.

Young Africans kupitia Afisa Habari Ally Kamwe amezungumzia ishu hiyo kwa kusema: “Bado uongozi unaendelea kupitia CV za makocha, hivyo kama taratibu zikishakamilika basi tutaweka wazi kila kitu.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad