Dar es Salaam. Mkazi wa Chanika, Jamal Mikome (48) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na shtaka moja la kutumia lugha ya matusi kuitukana Serikali iliyopoko madaraka.
Mikome, ambaye ni mfanyabiashara, alifikishwa mahakamani hapo, leo Jumatatu Juni 19, 2023 na kusomewa shtaka lake na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Neema Moshi akishirikiana na Erick Kamala mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Mary Mrio.
Wakili Mosha amedai kuwa mshtakiwa huyo anakabiliwa na kesi ya jinai namba 104/2023.
Akisomewa shtaka hilo, Wakili Moshi amedai mshitakiwa alitenda kosa hilo Aprili 28, 2023 eneo la Chanika, Wilaya ya Ilala.
Inadaiwa siku hiyo ya tukio na eneo hilo, alitumia lugha ya matusi kwa kuitukana Serikali iliyoko madaraka.
Inadaiwa kuwa mshtakiwa anadaiwa kutoa kauli hiyo kinyume na sheria za nchini.
Baada ya kusomewa shtaka hilo, mshitakiwa alikana na upande wa mashitaka ulidai upelelezi umekamilika, hivyo kuomba tarehe nyingine ya kutajwa.
Hakimu Mrio alitaja masharti ya dhamana kuwa mshitakiwa awe na mdhamini mmoja mwenye barua ya utambulisho kutoka Serikali ya mtaa atakayetia saini dhamana Sh3 milioni.
Hata hivyo, mshtakiwa yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti.
Hakimu Mrio ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 6, 2023 kwa ajili ya upande wa mashtaka kumsomea hoja za awali (PH), mshtakiwa