Mfanyabiashara Maarufu Tanga Ajinyonga na Waya wa Umeme Store, Mke Afunguka


Mfanyabiashara maarufu jijini Tanga anayejulikana kwa jina la Hamisi Rashid mwenye umri wa miaka 53 amejinyonga kwa kutumia waya wa umeme jana Juni 26, 2023, kwenye stoo ya nyumba yake baada ya kamba za katani kushindwa kumuua.
Mke mdogo wa marehemu huyo,Mwanaidi Isah, amesema kwamba mume wake usiku wa kuamkia jana alilala kwa mke wake mkubwa na aliporudi kwake alikuwa akilalamika kuwa tumbo linamuuma na baada ya hapo alimuagiza dukani akachukue sabuni lakini aliporudi alikuta mume wake huyo tayari kashajinyonga.

"Mume wangu alilala kule Donge kwa mke mwenzangu alfajiri alikuja kwangu hapa Makorora akilalamika kuwa tumbo linamuuma akanituma nikamletee sabuni dukani kwetu niliporejea nikamkuta stoo akiwa ameshajinyonga" amesema Mwanaidi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Henry Mwaibambe amesema bado wanachunguza chanzo kilichopelekea mfanyabiashara huyo kujinyonga.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad